SHADE pre and primary school ipo katika kata ya ibadakuli mkoani wa shinyanga. Shule ipo umbali wa KM 7 kutoka Manispaa ya Shinyanga. Shule ilianzishwa na kusajiliwa mnamo tarehe 19/11/2021 kwa namba za usajili EM 18928. Shule ni ya kutwa na ni moja ya miradi inayoendeshwa na shirika la SHADE lililopo mkoani Shinyanga. Taasisi ina maono thabiti ya kuwawezesha wanafunzi kufikia ubora wa kitaaluma na kuondoa changamoto za kiakili na kimwili na kuwafanya watoto wawe viongozi bora wa baadaye ili waweze kubadilisha dunia katika mtazamo chanya. Tunaamini watoto wakipata msingi bora watakuwa wawajibikaji katika jamii na hivyo kuwa na Taifa lenye nguvu.
Kwa bidii yetu yote tumeifanya kuwa dhamira yetu:
Hivyo basi maono haya tumeyakumbatia na kuweka nguvu kwa kila mfanyakazi wa Shule na shirika kutimiza maono haya kwa wanafunzi wetu, Shule itapata mafanikio makubwa sana kwa miaka mingi ijayo, ni dhamira yetu kuifanya SHADE kuwa uwanja wa kupumzika kwa watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu, kuibua viongozi wa Tanzania na Kimataifa.
Shule ya SHADE PRE AND PRIMARY SCHOOL ina kituo cha malezi na makuzi kwa Watoto wadogo kabla hawajaanza elimu ya Awali. Kituo kinajulikana kwa jina la SHADE DAY CARE CENTRE. Ni kituo cha kisasa cha malezi ya watoto kinachotoa huduma bora kwa watoto wadogo wenye umri wa miaka 3-4. Kituo hiki kimejikita katika kuhakikisha usalama, afya, na maendeleo ya kihisia, kijamii na kiakademia kwa watoto wanaolelewa chini ya uangalizi wetu. Kituo kimesajiliwa rasmi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu mnamo tarehe 3/9/2025. Kituo kimesajiliwa kwa namba 4389, Hivyo kituo kina vibali vya uendeshaji, na hutekeleza kanuni zote za usalama,afya, na ustawi wa mtoto kama zinavyolekezwa na wizara inayosimamia ustawi wa jamii
Katika utoaji wa huduma, tunahakikisha watoto wanapata:
Kupitia timu yetu ya walezi waliofunzwa, tunahakikisha kwamba kila mtoto anapokea uangalizi binafsi, upendo, na mwongozo unaochochea ukuaji chanya na maendeleo ya muda mrefu.
Kuibua viongozi, kubadilisha ulimwengu
Simu: +255763543456, +255744087584
Tovuti: www.shadetz.org
Barua pepe: school@shadetz.org
Ada zetu ni nafuu sana kwani tumezingatia ubora zaidi, kwa mwaka 2025 Shule ya SHADE ina madarasa saba yaani (awali) madarasa matatu na (msingi) madarasa manne (darasa la kwanza, la pili, la tatu, na darasa la nne).
| Jan – Mar | Apr – Jun | Jul – Sep | Oct – Dec |
| 325,000 | 325,000 | 325,000 | 325,000 |
| Jan – Mar | Apr – Jun | Jul – Sep | Oct – Dec |
| 375,000 | 375,000 | 375,000 | 375,000 |
Shule ya SHADE inatoa fursa nzuri ya mfuko wa ufadhili wa elimu kama kipaumbele kwa watoto wenye ualbino na wenye mazingira magumu na hatarishi katika manispaa ya Shinyanga, watoto hawa hupata elimu bora na bure kabisa kuanzia darasa la awali hadi darasa la 6.
Tunaamini katika elimu jumuishi hivyo SHADE haikuwaacha watoto wengine wanaoishi katika mazingira magumu mfano yatima, wanaoishi na mzazi mmoja, pia hawa watoto wanapata elimu bora na bure hadi watakapo maliza darasa la 6.
Ubora, Nidhamu na Upendo