Utangulizi

SHADE pre and primary school ipo  katika kata ya ibadakuli mkoani Shinyanga. Shule ipo umbali wa KM 7 kutokea manispaa ya mkoa wa shinyanga. Shule hii ilianzishwa na kusajiliwa 19/11/2021 kwa namba za usajili EM 18928. Shule hii ya kutwa ni moja kati ya miradi inayoendeshwa na shirika la SHADE lililopo mkoani SHINYANGA, kwa kuanzisha shule hii ya awali na msingi taasisi hii ina maono thabiti ya kuwezesha wanafunzi kufikia ubora wa kitaaluma na kuondoa changamoto za kiakili na kimwili na kuwawezesha, kuwafanya watoto wawe viongozi bora wa baadae ili waweze kubadirisha dunia katika mtazamo chanya, tunaamini watoto wakipata msingi bora watakua wawajibikaji katika jamii na hivyo kua na taifa lenye nguvu.

Kwa bidii yetu yote tumeifanya kuwa dhamira yetu:

  1. Kutoa elimu bora na jumuishi ambayo ni chimbuko la ukuaji wa kiakili, kiroho na kimwili. Kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi sahihi kutokana na mzingira, kuwasaidia na kukidhi mahitaji yao yote muhimu wawapo shuleni.
  2. Kukuza fikra zao pamoja bila kujali tofauti za mwanafunzi kwa kuwafanya wawe viongozi bora wa baadae ili waweze kubadirisha dunia.
  3. Kuanzisha mfuko wa ufadhili wa elimu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, ili wapate elimu bora bure.

Hivyo basi maono haya tumeyakumbatia na tumeweka nguvu kwa kila mfanyakazi wa shule na shirika kutimiza maono haya kwa wanafunzi wetu, Shule itapata mafanikio makubwa sana kwa miaka mingi ijayo, pia tunataka SHADE iweze kuwa uwanja wa kupumzika kwa watoto wenye mazingira magumu pia  kulea wataalamu na viongozi wa nchini Tanzania na kimataifa.

Kauli Mbiu

Kukuza viongozi, kubadirisha dunia

Mawasiliano

Simu: +255763543456, +255744087584
Tovuti: www.shadetz.org
Barua pepe: school@shadetz.org

Ada za Shule

Ada zetu ni nafuu sana kwani tumezingatia ubora zaidi, kwa mwaka huu 2023 shule ya SHADE ina madarasa matano yaani (awali) madarasa matatu na (msingi) madarasa mawili (darasa la kwanza na darasa la pili).

Awali

  1. Ada ya awali ni 500,000 kwa mwaka.
  2. Ukitaka usafiri wa basi la shule ni 900,000 kwa mwaka.
  3. Ada hii hulipwa mara mbili kwa mwaka, kila baada ya miezi 6.
  4. Malipo ya awamu ya kwanza hufanyika Januari na kama huna haja ya usafiri wa basi la shule ni 250,000 na baada ya miezi 6 utamalizia 250,000 kwa awamu ya pili.
  5. Malipo ya awamu ya kwanza hufanyika Januari, kama unahitaji usafiri wa basi la shule ni 450,000 na baada ya miezi 6 utamalizia 450,000.

Msingi

  1. Ada ya Elimu ya msingi ni 700,000 kwa mwaka.
  2. Ukitaka usafiri wa basi la shule ni 1,100,000 kwa mwaka.
  3. Ada hii hulipwa mara tatu kwa mwaka, (Januari, Juni na Septemba).
  4. Malipo ya awamu ya kwanza hufanyika Januari (450,000).
  5. Malipo ya awamu ya pili (450,000).
  6. Awamu ya tatu (200,000)

Mfuko wa ufadhili wa elimu kwa watoto wenye mazingira magumu

Shule ya SHADE inatoa fursa nzuri ya mfuko wa ufadhili wa elimu kama kipaumbele kwa watoto wenye ualbino wenye mazingira magumu na hatarishi katika manispaa ya Shinyanga, watoto hawa hupata elimu bora na bure kabisa kuanzia darasa la 1 hadi la 7.

Tunaamini katika elimu jumuishi hivyo SHADE haikuwaacha watoto wengine wanaoishi katika mazingiira magumu mfano yatima, wanaoishi na mzazi mmoja, pia hawa watoto wanapata elimu bora na bure hadi watakapo maliza darasa la 7.

Maneno ya kujenga misingi kwa watoto

Ubora, Nidhamu na Upendo